IQNA

Maulidi

Misikiti Misri yatayarishwa kwa ajili ya  sherehe za Maulidi

22:27 - September 12, 2024
Habari ID: 3479424
Misikiti ya IQNA – Misikiti nchini Misri ikiwemo ile inayonasibishwa na Ahl-ul-Bayt (AS), hususan Msikiti wa Imam Hussein (AS) na Msikiti wa Sayyidah Zainab (SA) mjini Cairo inatayarishwa kwa ajili ya sherehe za Milad-un-Nabi.

Sherehe za Maulidi au Milad un Nabi huadhimishwa kukumbuka kuzaliwa kwa Mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (SAW).

Kuwasha taa na kupamba misikiti na kuandaa vipindi vya usomaji wa Qur’ani Tukufu, Ibtihal na hotuba kuhusu Siira ya Mtukufu Mtume (SAW) ni miongoni mwa shughuli katika sherehe hizo.

Hadhirina katika misikiti pia hupewa keki, mandazi, na vinywaji vitamu.

Mustafa Abdul Salam, imamu na mhubiri wa misikiti ya Imam Hussein (AS) alisema Wamisri wanampenda Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na na huwaheshimu pia watu wa nyumba ya Mtume  (SAW) yaani Ahl-ul-Bayt (AS) na ni kunatokana na upendo huu ndio sherehe za Maulidi huadhimishwa kwa hadhi kubwa nchini humo.

Ameitaja siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) kuwa ni siku kubwa na yenye baraka na amewapongeza Waislamu wote kwa ujio wa hafla hiyo adhimu.

Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya watu wenye misimamo mikali wamepinga sherehe za Maulidi wakiita matukio hayo kuwa eti ni bidha na shirki.

Hata hivyo, wanazuoni wa Kiislamu katika nchi za Kiislamu kama vile Misri wameidhinisha sherehe hizo, wakisisitiza umuhimu wa kuheshimu hadhi ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

4236083

Habari zinazohusiana
captcha